USIKU WA USWAZI... WAKALI WA SINGELI, MDUARA KUTIKISA DAR LIVE

Msaga Sumu
Stori: Andrew Carlos
WAKALI wa nyimbo za Mduara, Singeli, Mchiriku na Bongo Fleva wanatarajiwa kutikisa leo (Aprili 23), ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar katika bonge la shoo lijulikanalo kama Usiku wa Uswazi.

JUMA nMkali wa Bongo Fleva, Juma Nature
Akizungumza na Risasi Jumamosi, mratibu wa shoo hiyo, Ester Kiama aliwataja wakali watakaotikisa leo kuwa ni pamoja na mkongwe wa Bongo Fleva, Juma Nature, mkali wa Mduara, Snura, mkali wa Mchiriku Msaga Sumu pamoja na mkali wa Singeli Man Fongo.
“Tutakuwa pia na Kibao Msambwanda ambapo mashabiki wote watakaofika watashuhudia nyonga zikikatwa laivu. Pia tutakuwa na mastaa kibao kutoka Bongo Muvi wakiongozwa na Gabo Zigamba,” alisema Ester.

GLOBAL PUBLISHERS

No comments