MASKINI, WATOTO WA MICHAEL JACKSON KUKOSA URITHI WA PAUNI 900 MILIONI
IMERIPOTIWA kwamba watoto watatu wa mfalme wa muziki wa pop duniani, marehemu Michael Jackson wako hatarini kukosa urithi mkubwa kutokana na kodi.
Watoto hao, Prince (19), Paris (17) na Blanket 914) walikuwa warithi rasilimali zenye thamani ya Paundi 900 milioni watakapofikisha miaka 30, lakini mamlaka zinadai kiasi cha Paundi 555 milioni kutokana na kodi za hekalu la Michael.
Inaaminika pia kwamba mwanamuziki huyo nguli, aliyefariki dunia mwaka 2009, alikuwa na madeni mengine yanayofikia Paundi 300 milioni ambayo yatakomba kiasi kingine kilichosalia katika urithi wa watoto hao.
Chanzo kimoja kililieleza gazeti la The Sun: “Kwenye makaratasi watoto hao ni mabilionea kutokana na kiasi hicho kikubwa cha mali. Lakini ukweli ni kwamba kiasi hicho hakitaendelea kuwa mikononi mwao kutokana na madeni makubwa na kodi.
“Idara ya Kodi za Ndani (Internal Revenue Service) imesema wazi kwamba inataka kiasi cha Paundi 555 milioni, na deni linaweza kuongezeka ikiwa halitalipwa kwa wakati.”
Kodi hiyo ilipanda ghafla kwa kiasi cha Paundi 70 milioni baada ya hisa za Michael katika kampuni ya Sony/ATVMusic Publshing kuuzwa wiki iliyopita kwa Paundi milioni 526, huku chanzo cha ndani kikiongeza: “Himaya ya Michael imepinga kiasi hicho kikubwa, lakini dili la Sony limeongeza deni wanalodaiwa.”
Lakini si hicho tu ambacho watoto wa Jackson wamepoteza, kwani kuna taarifa kwamba tuzo ya Oscar ya ‘Gone With The Wind’ ambayo staa huyo aliinunua kwa Dola 1.54 milioni mwaka 1999, imepotea.
Wasimamizi wa mali za Michael wameshindwa kuipata tuzo hiyo na hawajui ni wapi nyota huyo aliiweka, huku Mwanasheria Howard Weitzman akikiri: “Hakuna anayejua ile sanamu ya ‘Gone With the Wind’ ilipo. Tungependa tuipate Oscar kwa sababu inastahili kumilikiwa na watoto wake. Ninatumaini itakuja kuonekana tu.”

Post a Comment