HAITHAM... ZAO JIPYA LA MJ RECORDS


MZIKI wa Bongo Fleva unazidi kukua kila kukicha, Msanii Chipukizi wa Bongo Flava, Haitham Ghazal Seif “Haitham” ametoa ngoma yake ya kwanza aliyomshirikisha rapa mkongwe wa Bongo Flavani, Mwana FA katika ngoma inayoitwa Fulani.
Ngoma hiyo ya Haitham aliyomshirikisha Mwana FA (Fulani) imetengenezwa na Daxo Chali ambaye ni mdogo wa Marco Chali chini ya kwenye studio za MJ Records.
Akipiga stori na mtandao huu, prodyuza aliyetengeneza ngoma hii (Daxo Chali) alisema; “Huyo Haitham ni msanii mpya kwenye game, anafanya vizuri sana, ndiyo maana sisi kama MJ records tukaamua kumchukua na kumsainisha kwenye lebo yetu, kwa wasanii wetu wa MJ huyu ndiyo yupo katika uangalizi zaidi kwa sasa”
“Nachoweza kusema, tumewekeza nguvu, akili na maarifa yetu kwa msanii huyu ili kumsaidia na tunaamini atafika mbali kimziki kama na yeye ataendelea kuipenda kazi yake na kujituma kwa bidii kama anavyofanya sasa hivi.”
Kuhusu kichupa cha Fulani vipi?
Daxo Chali aliendelea kufunguka; “Video imekamilia tayari, kwa hiyo kinachosubiliwa ni siku ifike, maandalizi yameshafanyika na video tunatarajia kuichia Jumatatu ya keshokutwa (Aprili 25, 2016) lakini mitandaoni hasa YouTube itaanza kuonekana kuanzia Ijumaa ya wiki ijayo (Aprili).
Haitham anasemaje?
Kwa nini umshirikishe Mwana FA na siyo msanii mwingine; “Kwanza kabisa, aina ya Bongo Fleva ninayoimba mimi ni mpya, unaitwa Tropical House. Baada ya mimi kumaliza kuingiza vocal kwenye ngoma hiyo, kulingana na aina ya wimbo wenyewe, menejimenti yangu ilipendekeza Mwana FA ‘akae’ kwenye ngoma hiyo ndipo itanoga zaidi.”
Kuhusu usambazaji wa Video
Kampuni yangu imeingia mkataba na Kampuni ya Africori ya Kenya ambayo itahusika kusambaza ngoma hiyo.
Isikie Video

CREDIT: RISASI JUMAMOSI

No comments