HAMISA MOBETO ANASA MTUNGO WA MKONGO!
Mwanamitindo na staa wa Bongo Movie, Hamisa Mobeto.
Stori: Mwandishi Wetu, Ijumaa
DAR ES SALAAM: Baada ya mpenzi wake kunyakuliwa na staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mwanamitindo Hamisa Mobeto amedaiwa kuingia kwenye penzi la mfanyabiashara Mkongo, Mwami Rajabu ambaye ana msururu mrefu wa mastaa aliowahi kudaiwa kutoka nao.

Kabla ya kumnasa Mobeto, Mkongo huyo ameshawahi kuripotiwa kutembea na mastaa warembo tofauti Bongo akiwemo Husna Maulid, Jacqueline Wolper, Agnes Gerald ‘Masogange’, Tunda Sabastian na Wema Sepetu.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Hamisa alianzisha uhusiano wa siri na Mkongo baada tu ya mzazi mwenzie ambaye ni bosi wa redio moja jijini Dar kunyakuliwa na Lulu, hivyo kujipoza machungu kwa Mkongo.
Chanzo hicho makini kilizidi kushibisha ubuyu huo wa motomoto kwa kupenyeza meseji walizokuwa wakitumiana Hamisa na Mkongo ambazo baadhi yeke ziliashiria kabisa kuwepo na uhusiano baina yao hadi kusababisha ugomvi kati ya mrembo huyo na Husna Maulid ambaye bado anaitamani nafasi kwa Mkongo.
“Jamani najua Hamisa atakuwa tu alichanganywa na yule baba mtoto wake kwenda kuhamishia penzi kwa Lulu hivyo akaamua aende kwa Mkongo ambaye anaamini angeweza kumsaidia maana ilifikia kipindi wakawa hawaelewani na Husna Maulid kabisa aliposhtukia mchezo,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
Tunda Sabastian.
Tunda Sabastian.
“Huyu Mkongo mwenzangu si bure, atakuwa anatumia ‘kamzizi’ kuwanasa hawa mastaa maana msururu wake sasa ni mkubwa na bado kuna ambao hawajaandikwa gazetini lakini wapo kwenye listi yake.”
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa, Hamisa alipoona hakuna tena mapenzi yanayoweza kuendelea kati yake na mzazi mwenziye aliamua kuendelea na maisha yake na kuzidi kujiimarisha kimahaba kwa Mkongo.

Ili kuweka usawa wa habari, gazeti hili lilimsaka kwa njia ya simu Hamisa ambapo alipoulizwa kuhusu ishu hiyo, alisema:Mkongo akipozi kimahaba na Hamisa Mobeto.
“Jamani mimi ningependa niachwe kwa kuwa mimi ni mama wa familia, nisingependa kuingizwa kwenye mambo hayo.”
Baada ya Hamisa kuomba aachwe licha ya kuambiwa kuna ushahidi wa meseji zake za kimahaba na Mkongo, Ijumaa lilimuendea hewani Mwami ili kumsikia anazungumza nini kwa upande wake:
Ijumaa: Vipi Mwami, Gazeti la Ijumaa hapa naona siku hizi mapenzi umehamishia kwa Hamisa.
Ijumaa: Vipi Mwami, Gazeti la Ijumaa hapa naona siku hizi mapenzi umehamishia kwa Hamisa.
Mkongo: Hivi kwa nini mnapenda kunifuatafuata?
Ijumaa: Siyo hivyo kuna meseji zenu tumezinasa hapa, zinaonesha wewe unachati na Hamisa, pengine ungetueleza ndiyo ameshikilia usukuni kwa sasa au la?
Ijumaa: Siyo hivyo kuna meseji zenu tumezinasa hapa, zinaonesha wewe unachati na Hamisa, pengine ungetueleza ndiyo ameshikilia usukuni kwa sasa au la?
Husna Maulid.
Mkongo: Sasa mimi nifanyeje mkizinasa hizo meseji?
Ijumaa: Ndiyo maana tunataka kujua sasa hivi mko wote?
Mkongo: Hizo meseji zinaonesha mimi namsumbua Hamisa au yeye ndiyo ananisumbua mimi?
Ijumaa: Inaonekana wote wapenzi.
Mkongo: Naomba achaneni na mimi tafadhali.(akakata simu)
Kwenye meseji hizo mbali na kuonesha Hamisa akimuita baby Mkongo, kuna sehemu mrembo huyo ameonekana akimuomba mkwanja.

“Na ombi langu? Maana natakiwa nikalipie mapazia now nafanyaje? Kwa sababu na pesa si lazima nizifuate. Or nazipataje sasa? Nasubiria jibu lako…”
CREDIT: GPL
Post a Comment